NEWS

Ijumaa, 18 Oktoba 2013

HAJI RAMADHANI ANG'ARA UPYA KWENYE KIPINDI KIPYA CHA " STAR'S TALK"


                                            mtangazaji Shufaa akimuhoji Haji Ramadhani
                                             mtangazaji Jonh akimuhoji Haji Ramadhani
                                          camera men shooting Haji's Interview
                                                    cameramen wakipiga picha na  Haji Ramadhani
                                             production na Haji Ramadhani
                                          Presenters crew na Haji Ramadhani
Msanii mkubwa wa muziki wa kizazi kipya pia muziki wa dance ambaye ni zao la BSS Bongo Star search mshiriki alietikisa sana 201maarufu kwa jina la Haji Ramadhani, ang'ara upya baada ya kuwa kimya kidogo kwakufanya  bonge moja la interview na  kipindi kikubwa cha Star talk ambacho kina husu msanii kuongea.
Haji amekuja amefunguka mengi ambayo wengi atuyajui na kusema yamoyoni kuhusu Nei Wamitego na  mengi ya husuyo muziki kwa ujumla ,pia amejibu kama nangependa kutika na staa au la.....
katayari kwa interview hiyo itakayo rushwa humu pia karibuni. 

Jumanne, 8 Oktoba 2013

BIRTHDAY YA Dar29 YAFUNIKA MSASANI BEACH.

Philip Nyiti(mwenye shati jeupe)  akiwa anakata keki,weweeee!
Matukio katika picha mchanganyiko yakionesha washiriki na waandishi wa Dar29 wakishelekea uzinduzi wa siku ya kuzaliwa kwa Blog hiyo(Dar29) ilikuwa ni shangwe tupu!!!!!!


Na: John Julius
           Ilikuwa ni jumamosi ya tarehe 5/10/2013 katika fukwe za Msasani Beach ambapo waandishi wa Dar29 na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari walipojumuika kwa pamoja kusherekea kuzaliwa kwa blog ya Dar29.
           Sherehe hizo zilizoanza muda wa saa 4 aubuhi katika chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam School of Journalism(DSJ) zilizoambatana na shamrashamra za kuzaliwa kwa mmoja wa waandishi wa Blog hiyo ya Dar29
 Bw, Philip Nyiti ambaye alikuwa akitimiza umri wa miaka 18.Baada ya hapo shamrashamra hizo ziliamia katika fukwe za Msasani Beach mida saa nane(8) mchana ambapo ilikatwa keki ya Dar29 na kufungua Champagne.
          Baada ya hapo watu walijichanganya ndani ya maji na kuanza kupiga mbizi,wengine wakitembea na kucheza michezo mbalimbali kando ya fukwe hizo,michezo kama beach soccer na mpira wa mikono ilihusika kwa sana.
             

VUGUVUGU LA UCHAGUZI WA DASJOSO LAANZA KURINDIMA DSJ.

VUGUVUGU LA UCHAGUZI WA DASJOSO  LAANZA KURINDIMA DSJ.

Na: Philip Nyiti
Ikiwa siku chache baada ya wagombea wa urais wa serikali ya wanafunzi DASJOSO katika chuo cha uandishi wa habari DSJ kurudisha fomu siku ya jana katika ofisi kuu za DASJOSO zilizopo ilala Sharifshamba mkabala na baraza la sanaa Tanzania(BASATA).Vuguvugu hili limezidi kuteka hisia za watu hasa baada ya wagombea wawili waliokuwa madarakani katika uongozi ambao muda wake unaisha kujihusisha na mchakato huo kwa kugombea nafasi za juu zaidi katika serikali ya wanafunzi ambazo ni Rais na Makamu wa rais.Viongozi hao ambao ni  Mhe.Magesa Laurean Marwa ambaye alikuwa katibu mkuu wa serikali ya wanafunzi(DASJOSO) na aliyekuwa spika wa bunge Mhe.Norbert Laurent. Magesa Marwa ambaye anagombea makamu wa rais na Norbert Laurent Maloko  ambaye anagombea kiti cha uraisi katika serikali hiyo wameonyesha kuteka hisia za wanafunzi wa chuo hicho hasa baada ya kuwa na wakati mzuri kipindi wapo katika serikali ambayo inamaliza muda wake mwezi wa kumi mwaka huu.Wagombea wengine kwenye uchaguzi huo ni James Mwakibinga ambaye nae anaogombea nafasi ya Urais na Asma Bashir ambaye anagombea umakamu wa Rais. Kulingana na taarifa iliyotolewa na tume ya uchaguzi tarehe 9/10/2013  siku ya jumatano ndio itakuwa siku ya ufunguzi wa upigaji kampeni kwa wagombea vivyo hivyo tume imetoa angalizo kwa viongozi na walimu kutojihusisha na kuwapigia kampeni wagombea na kanuni za kinidhamu zitachukuliwa kwa yoyote ambaye atabainika kuwapigia kampeni.
Magesa Laurean Marwa( kushoto) na Norbert Laurent( kushoto)

1 comment: