Kiongozi wa wapiganaji wa M23
mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ametangaza kuwa watasitisha
mapigano katika vita vyao na jeshi la serikali.
Bertrand Bisimwa alisema kwenye taarifa kwamba
anawasihi wapiganaji wote haraka waache uhasama na wanajeshi, ili
kuwezesha mazungumzo ya amani kuendelea.Wanajeshi wa serikali, wakisaidiwa na kikosi cha kuweka amani cha Umoja wa Mataifa, hivi karibuni wamewasukuma nyuma wapiganaji na kuwatoa katika ngome zao nchini.
Mazungumzo ya amani yanafanywa mjini Kampala, Uganda.
No comments:
Post a Comment