Tuesday, November 5, 2013

Congo yawamaliza waasi wa M23

 
Lambert Mende Msemaji wa serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema majeshi yake kwa kushirikiana na kile kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupambana na waasi wa M23 kimewapiga waasi hao katika ngome yao ya mwisho.
Msemaji wa Serikali Lambert Mende ameiambia BBC kuwa wapigani waliobaki wa M23 wanaweza wakawa wamekimbia , wamevuka mpaka au wamejisalimisha.
Mende amesema kikosi maalum cha majeshi ya nchi hiyo kimeharibu silaha za waasi hao usiku kucha na inasadikiwa kiongozi wa kijeshi wa kundi hilo la M23 Sultani Makenga ni miongoni mwa waliovuka mpaka na kuingia Rwanda au Uganda.
Wakati huo huo viongozi wa nchi za SADC wanaokutana nchini Afrika Kusini wamezunguzia mgogoro wa Jumuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuwataka viongozi kundi la waasi wa M23 kutangaza kusimamisha mapigano.
Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo imesema kama waasi hao watachukua hatua hiyo mkataba wa amani unaweza kusainiwa ndani siku tano zijazo.

No comments:

Post a Comment