Na Mwandishi wetu
Dar es salaam
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa
habari Dar es salaam(DSJ) walisimamisha shughuli zote za Mkoa wa tanga hivi karibuni mara baada ya kufanya ziara ya kimasomo Mkoani humo wiki iliyopita.
Akizungumza na Blog hii katika mahojiano maalumu yaliyo fanyika Mkoani humo, aliyekuwa Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Mhe. Norbert Laurent Maloko alisema kuwa watakuwa mkoani hapo kwa takribani juma moja kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma ikiwa ni pamoja na kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo mkoani Tanga na Vyombo vya habari."Tutakuwa hapa Tanga kwa juma moja kwa lengo la kujifunza katika ziara yetu ya kimasomo na pia tutatembelea maeneo mbalimbali kama Bandari ya Tanga, Hospitali ya mkoa Bombo, Tanga Television, Mapango ya Amboni, Magofu ya Tongoni, Kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh pamoja na maeneo mengine mbalimbali.
Hii ni kawaida kwa Chuo cha DSJ kufanya ziara za kimasomo katika mikoa mbalimbali nchini na hata nje ya nchi kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma na pia kuangalia fursa za ajira maeneo husika.
|
Baadhi ya walimu na kiongozi wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho walioambatana na wanafunzi wakiwa katika magofu ya Tongoni Mkoani Tanga.Kutoka kushoto na Madam Stella Msaliboko, Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Magesa Marwa na Mwl. Malika Nginilla. | |
|
|
Msimamizi wa Kituo cha Magofu ya Tongoni akiwaelezea wanafunzi wa Dsj historia ya Magofu hayo. |
|
Kiwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh kilichopo Mkoani Tanga ambapo wanafunzi wa Dsj walikitembelea. |
|
Mmoja wa wanafunzi wa Dsj Elia Joseph akiwa katika studio ya Radio Ihsaani iliyopo Mkoani Tanga mara baada ya Wanafunzi hao kuitembelea hivi karibuni. |
|
|
Baadhi ya wanafunzi waDSJ maarufu kama 5 BEST FRIENDS wakiwa katika picha ya pamoja Mkoani Tanga walipokuwa ziarani mkoani humo hivi karibuni. |
|
Mwanafunzi wa Dsj Salumu akiwa katika Mapango ya Amboni Mkoani Tanga hivi karibuni. |
|
5 BEST FRIENDS wakiwa katika picha ya pamoja na Mkufunzi wao Ndugu. Malika Nginilla wakati wa ziara yao ya Kimasomo kwenye mapango ya Amboni. Kutoka kulia ni Rose msomba, Amina Mshana, Henrietha Mujumuzi na Angelina. |
|
5 BEST FRIENDS katika pozi tofauti Maeneo ya Chumbageni Mkoani Tanga wakati wa ziara ya kimasomo mkoani humo. |
No comments:
Post a Comment