Thursday, November 13, 2014

UPENDO KWA MUMEWE WAMTIA JELA

Amal El-Wahabi akiwa katika picha

 Mwanamke mmoja nchini Uingereza aliyeshitakiwa kwa kumfadhili mumewe aliyejiunga na vita nchini Syria, amefungwa jela kwa zaidi ya miaka miwili.Amal El-Wahabi, mwenye umri wa miaka 28, alijaribu kumhadaa rafiki yake kumbebea pauni 15,800 hadi nchini Uturuki ambako mumewe angeweza kuzichukulia.
Jaji aliyetoa uamuzi katika kesi hiyo, Nicholas Hilliard, alimwambia El Wahabai kuwa alifahamu vyema kwamba mumewe Aine Davis alikuwa anapigana nchini Syria na kwa hivyo alikuwa anamsaidia katika harakati zake.
Davis, ambaye alikuwa mlanguzi wa dawa za kulevya pamoja na kushtakiwa kwa kosa la kumiliki silaha, aliondoka Uingereza mwaka 2013 kwenda Syria kupigana na kundi la Isis.
Jaji alisema kuwa El-Wahabi anapaswa kutumikia sehemu ya kifungo chake jela na kabla ya kuachiliwa kumalizikia kifungo hicho nje.
Jaji aliongeza kusema kuwa uamuzi huo ulitolewa kwa huruma kwani mwanamke huyo ni mama wa watoto wawili wachanga.
Mapema mwaka huu Davisa ambaye anajulikana kama Hamza alimtaka mkewe kumtumia pesa hizo kupitia nchini Uturuki.
El-Wahabi, kutoka London alimuomba rafiki yake wa zamani, Nawal Msaad,kumbebea pesa hizo akimuahidi kumlipa Euro 1,000 kwa kumshukuru.
Hata hivyo, mpango huo ulitibuka baada ya Msaad kusimamishwa katika uwanja wa Heathrow na kukiri ni kweli alikuwa amebeba pesa hizo. Pesa hizo alikuwa amzificha kwa nguo zake za ndani.
Bi Msaad alisema hakujua pesa hizo zilikokuwa zinakwenda na kwa hilo mahakama ikamwachilia.
Katika hukumu yake jaji alisema ni wazi kuwa mumewe El-Wahabi alikwenda Syria kupigana chini ya kundi la kiisilamu la Isis.

GARI ISIYOTUMIA PETROLI YAZNDULIWA UGANDA

 

Nchi yaUganda imezindua gari maalum la kipekee katika kanda ya Afrika mashariki maarufu kama hybrid electric car.
Uzinduzi wa gari hilo ulifanyika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Lakini je, hybrid electric car ni gari la aina gani? Hili ndilo swali mwandishi wetu, Wanyama wa Chebusiri amemuuliza mmoja wa wahandisi waliotengeneza hilo gari, Bwana Mario Obua..

QATAR UFISADI WAIKWEPA

Mkuu wa shirikisho la Soka Duniani(FIFA) Bw. Sepp Blatter


Maafisa wa Qatar wakisherehekea ushindi wa kuandaa kombe la dunia mwaka 2022
Shirikisho la soka duniani FIFA limeilaumu shirikisho la soka la Uingereza kwa kuvunja sheria za kutolewa kwa kibali cha kuandaa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018.
Lakini shirikisho hilo limeiondolea Qatar lawama za rushwa wakati wa kupigania zabuni za kuandaa kombe la dunia mwaka 2022.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirikisho hilo, shirikisho la soka la Uingereza ilikwenda kinyume na utaratibu katika juhudi zake kutaka kupata nafasi ya kuandaa michuano ya kombe la duniani mwaka 2018.
Lilifanya hivyo ili kupata kura ya mmoja wa washawishi.
Kwa upande ake Qatar ilikabiliwa na tuhuma nyingi tu, lakini taifa hilo sasa liko huru kuandaa michuano hiyo.
Kwa sasa ripoti iliyotolewa na FIFA inamaliza mgogoro kuhusu ikiwa kura nyingine itapigwa kuteua waandaji wa mashindano hayo katika miaka hiyo.
FIFA imeelezea kuwa mambo sasa yako shwari kufuatia uamuzi huo.
Qatar ilituzwa kuandaa kombe la duna mwaka 2022 mnamo 2010 na kuyapiku mataifa ya Australia, Marekani,Korea Kusini na Japani.
Uamuzi ulishangaza wengi na mwishowe kupelekea madai kadhaa ya rushwa, sio tu kuhusu mchakato wa zabuni za 2022 bali pia 2018.
Urusi ilishinda zabuni ya kuandaa mashindano ya mwaka 2018 na kuishinda Uingereza ambayo ilipata kura mbili pekee.
Qatar daima imekataa madai ya kufanya kosa, lakini uchunguzi ulianzishwa ukiongozwa na mchunguzi huru wa nidhamu Michael Garcia.
Mwanasheria huyo, raia wa Amerika pia alipewa kazi ya kuchunguza michakato ya zabuni ya kombe la dunia ya 2018 na 2022.

MJAMZITO CHUPUCHUPU KUPIGWA BEI

Sehemu ya Urembo wanaorembwa Maharusi wa kike


Watu kumi na watatu wamekamatwa kufuatia sakata ya biashara haramu ya binadamu ambapo nusura mwanamke mjamzito kuhadaiwa kutoa mimba yake kufuatia mpango wa kumuoza kwa lazima kutibuka.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 20 kutoka Slovakia, aliuzwa kwa kima cha pauni, 15,000 na genge la wahalifu katika mtaa wa Great Macheseter.
Genge hilo lilimpangia mwakamke huyo kuolewa na mwanamume mmoja aliyekuwa anasubiri kutimuliwa kutoka nchini Uingereza kwa kuwa nchini humo kinyume na sheria.
Maafisa wa polisi walipokea taarifa kutoka kwa mwanamke huyo pale alipomwambia mkalimani kuwa aliozwa kinyume na matakwa yake na kwamba alichukizwa sana na pandekezo kuwa atoe mimba yake.
Wanaume kumi na wanawake watatu walikamatwa kufuatia kashfa hiyo.
Wahalifu hao walikuwa kati ya umri wa miaka 24 na 57 na walikamatwa kwa tuhuma za kushiriki biashara haramu ya kuwauza watu pamoja na kuwa na njama ya kuvunja sheria za uhamiaji.
Mnamo mwezi Mei, mwanamke huyo aliyekuwa na ujauzito wa wiki 25 alipelekwa katika mtaa wa Luton akidhani alikuwa anakwenda kuwatembelea jamaa wake.
Hapo ndipo alikutana na mwanamume mmoja aliyedai kuwa rafiki ya dadake na ambaye alimpeleka kwa mwanamume mmoja ambapo walimuoza kwa lazima mnamo mwezi Julai chini ya sheria ya kiisilamu katika mtaa wa Rochdale.
Baadaye mwanamke huyo alipelekwa hospitalini na rafiki mmoja wa dadake ambaye aliambia maafisa wa hospitali kuwa alitaka kutolewa mimba.
Polisi waligundua kuwa mwanamke huyo kwanza aliolewa kwa lazima na pili kukawa na mpango wa kumtoa mimba yake kwa lazima.
Polisi wanasema kuwa kuna visa vingi vya wanawake kuozwa kwa lazima na kuuzwa kama bidhaa nchini Uingereza.Visa vya kuwaoa wanawake kwa lazima huripotiwa sana nchini Uingereza

LIBYA KWACHAFUKA TENA

 
Baadhi ya wananchi wa Libya wakiangalia gari iliyolopuliwa na Bomu
Misri imelaumiwa kwa kuchochea mashambulizi hayo kutokana na harakati zake dhidi ya makundi ya kiisilamu
Habari kutoka katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, zinasema kuwa mabomu mawili ya kutegwa ndani magari yamelipuliwa , moja karibu na ubalozi wa Misri na jingine karibu na ubalozi wa milki za kiarabu .
Balozi zote hizo mbili zimefungwa kwa miezi kadhaa .
Hakuna taarifa kuhusu majeruhi kufuatia mashambulizi hayo.
Makundi ya kiislam yanayodhibiti mji mkuu awali yaliishutumu Misri kwa kuanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya vikosi vya kiislam nchini Libya , shutuma ambazo zimekabushwa na serikali ya Misri.
Wakati huo huo Misri imeyashutumu makundi ya wapiganaji ya Libya kuwasaidia wapigganaji wa kiislam wa Misrui katika rasi ya Sinai.

DAKTARI ALIYESABABISHA VIFO VYA WANAWAKE ATIWA MBARONI


Mmoja wa wagonjwa wanawake waliozidiwa akiwa hoi hospitalini hapo
 Ikiwa ni siku mbili baada ya kupewa huduma ya kuzuia uzazi kwa njia ya upasuaji wanawake nchini India, Daktari anayehusishwa na tukio la vifo vya watu 13 katika kituo kilichokua kikitoa huduma ya kuzuia uzazi kwa njia ya upasuaji jimboni Chattisgarh nchini India,amekamatwa.
Dokta RK Gupta na msaidizi wake waliwafanyia upasuaji wananawake 83 katika kijiji cha Pendari.
Ripoti zinasema Daktari huyo aliwafanyia upasuaji wanawake 83 kwa saa tano, Serikali inasema Daktari mmoja anapaswa kutoa huduma ya upasuaji kwa Watu 35 kwa siku.
Wanawake wengine wawili walipoteza maisha baada ya kufanyiwa uapsuaji huo.
Zaidi ya wanawake 90 wako hospitalini wengi wao wakiwa katika hali mbaya,baada ya upasuaji.
Maandamano yamefanyika baada ya tukio la vifo , Serikali ya jimbo la Chhattisgarh imetoa amri ya kufanyika kwa uchunguzi,bado haijafahamika chanzo cha vifo hivyo.
Maafisa wa afya jimboni humo wamekana kuhusika na tukio hilo, lakini baadhi yao wamesema walikua katika hali ya kushinikizwa na mamlaka kufanya operesheni nyingi kwa muda mfupi.



HUU NDIO UGONJWA WA TEZI DUME

Ikiwa  ni siku rchache baada ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kufanyiwa upasuaji wa Tezi dume huko Nchini Marekani... Basi leo pata  Makala fupi ili kujua jinsi ugonjwa huu wa Tezi dume unavyokuwa.
 
                                                Kielelezo cha Mchoro wa tezi dume(Prostate gland)

TEZI DUME NI NINI?

 
Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na uume (urethra).

Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu.

Kuvimba Tezi Dume (BPH)
Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho huu wa BPH ili kurahisisha mambo.

Ukuaji wa tezi dume hupitia hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali. Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka 25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha
BPH katika umri wa utu uzima.

Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu.

BPH husababishwa na nini?
Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa PBH haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja na uwepo wa korodani.

Wednesday, November 5, 2014

MATOKEO YA DARASA LA SABA SHULE ZA MKOA WA MARA

BONYEZA HAPO CHINI KUYAANGALIA.

DSJ WATIKISA JIJI LA TANGA

Na Mwandishi wetu
Dar es salaam

Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Dar es salaam(DSJ) walisimamisha shughuli zote za Mkoa wa tanga hivi karibuni mara baada ya kufanya ziara ya kimasomo Mkoani humo wiki iliyopita.

Akizungumza na Blog hii katika mahojiano maalumu yaliyo fanyika Mkoani humo, aliyekuwa Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho Mhe. Norbert Laurent Maloko alisema kuwa watakuwa mkoani hapo kwa takribani juma moja kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma ikiwa ni pamoja na kutembelea vivutio mbalimbali vilivyomo mkoani Tanga  na Vyombo vya habari."Tutakuwa hapa Tanga kwa juma moja kwa lengo la kujifunza katika ziara yetu ya kimasomo na pia tutatembelea maeneo mbalimbali kama Bandari ya Tanga, Hospitali ya mkoa Bombo, Tanga Television, Mapango ya Amboni, Magofu ya Tongoni, Kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh pamoja na maeneo mengine mbalimbali.
Hii ni kawaida kwa Chuo cha DSJ kufanya ziara za kimasomo katika mikoa mbalimbali nchini na hata nje ya nchi kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya kitaaluma na pia kuangalia fursa za ajira maeneo husika.


Baadhi ya walimu na kiongozi wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho walioambatana na wanafunzi  wakiwa katika magofu ya Tongoni Mkoani Tanga.Kutoka kushoto na Madam Stella Msaliboko, Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Magesa Marwa na Mwl. Malika Nginilla. 
Msimamizi wa Kituo cha Magofu ya Tongoni akiwaelezea wanafunzi wa Dsj historia ya Magofu hayo.

 



Kiwanda cha Maziwa cha Tanga Fresh kilichopo Mkoani Tanga ambapo wanafunzi wa Dsj walikitembelea.


Mmoja wa wanafunzi wa Dsj Elia Joseph akiwa katika studio ya Radio Ihsaani iliyopo Mkoani Tanga mara baada ya Wanafunzi hao kuitembelea hivi karibuni.



Baadhi ya wanafunzi waDSJ maarufu kama 5 BEST FRIENDS wakiwa katika picha ya pamoja Mkoani Tanga walipokuwa ziarani mkoani humo hivi karibuni.



Mwanafunzi wa Dsj Salumu akiwa katika Mapango ya Amboni Mkoani Tanga hivi karibuni.


5 BEST FRIENDS wakiwa katika picha ya pamoja na Mkufunzi wao Ndugu. Malika Nginilla wakati wa ziara yao ya Kimasomo kwenye mapango ya Amboni. Kutoka kulia ni Rose msomba, Amina Mshana, Henrietha Mujumuzi na Angelina.


5 BEST FRIENDS katika pozi tofauti Maeneo ya Chumbageni Mkoani Tanga wakati wa ziara ya kimasomo mkoani humo.