Ikiwa ni siku rchache baada ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kufanyiwa upasuaji wa Tezi dume huko Nchini Marekani... Basi leo pata Makala fupi ili kujua jinsi ugonjwa huu wa Tezi dume unavyokuwa.
|
Kielelezo cha Mchoro wa tezi dume(Prostate gland)
TEZI DUME NI NINI?
Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Inaundwa na
sehemu mbili, lobes, ambazo zimeunganishwa na kufunikwa kwa nje kwa
utando wa tishu. Tezi hii ipo mbele kidogo ya puru (rectum) na na chini
kidogo ya kibofu cha mkojo. Tezi dume inauzunguka mrija unaounganisha
kibofu cha mkojo na uume (urethra).
Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na
mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono.
Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa
(semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya
kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa
utungisho na yai la kike. Vilevile husaidia kupunguza hali ya
kitindikali iliyopo katika uke, ambayo kama isiporekebishwa, huweza kuua
mbegu nyingi za kiume na kufanya utungisho kuwa wa tabu. Kuvimba Tezi Dume (BPH)
Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume
kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate
Hyperplasia au wengine hupenda kutumia maneno Benign Prostate
Hypertrophy kwa kifupi BPH. Kwenye makala hii tutautumia sana ufupisho
huu wa BPH ili kurahisisha mambo. Ukuaji wa tezi dume hupitia
hatua kuu mbili. Hatua ya kwanza hutokea kipindi cha balehe wakati tezi
dume linapoongezeka ukubwa na kuwa mara mbili ya lilivyokuwa hapo awali.
Baada ya hapo ukuaji husimama kwa muda mpaka kijana anapofikisha miaka
25 hadi 30 ndipo hatua ya pili ya ukuaji huanza tena. Ukuaji huendelea
kwa viwango na kasi tofauti kati ya mtu na mtu na hatimaye kusababisha BPH katika umri wa utu uzima.
Wakati tezi dume linapokua na kutanuka, utando wa tishu unaozulizunguka
hutanuka pia. Hata hivyo ingawa tezi dume huendelea kukua, hufikia
wakati utando wake huacha kutanuka na kufanya tezi dume kubana mrija wa
kutolea mkojo kutoka kwenye kibofu. Hali hii husababisha kibofu cha
mkojo kuwa na ngozi ngumu. Hali hii hufanya kibofu cha mkojo kuhisi
kutaka kutoa mkojo nje hata kama kiasi cha mkojo ndani yake ni kidogo
sana. Hufikia wakati, kibofu huwa dhaifu na kupoteza uwezo wake wa
kuhisi kutoa mkojo na hivyo kufanya mtu anapokojoa kushindwa kutoa mkojo
wote na badala yake hubakiza kiasi fulani cha mkojo kwenye kibofu. BPH husababishwa na nini?
Chanzo halisi cha BPH au vihatarishi vyake (risk factors) havijulikani
kwa uhakika. Kwa muda mrefu imekuwa ikichukuliwa kuwa BPH hutokea kwa
wanaume watu wazima na wazee tu. Aidha imewahi kuonekana huko nyuma kuwa
PBH haitokei kwa wanaume ambao wamewahi kufanyiwa operesheni ya kuondoa
korodani au wale ambao walizaliwa bila korodani. Hali imepelekea baadhi
ya watafiti kuamini kuwa BPH ina uhusiano mkubwa na umri wa mtu pamoja
na uwepo wa korodani.
|
No comments:
Post a Comment