Thursday, November 13, 2014

QATAR UFISADI WAIKWEPA

Mkuu wa shirikisho la Soka Duniani(FIFA) Bw. Sepp Blatter


Maafisa wa Qatar wakisherehekea ushindi wa kuandaa kombe la dunia mwaka 2022
Shirikisho la soka duniani FIFA limeilaumu shirikisho la soka la Uingereza kwa kuvunja sheria za kutolewa kwa kibali cha kuandaa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018.
Lakini shirikisho hilo limeiondolea Qatar lawama za rushwa wakati wa kupigania zabuni za kuandaa kombe la dunia mwaka 2022.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirikisho hilo, shirikisho la soka la Uingereza ilikwenda kinyume na utaratibu katika juhudi zake kutaka kupata nafasi ya kuandaa michuano ya kombe la duniani mwaka 2018.
Lilifanya hivyo ili kupata kura ya mmoja wa washawishi.
Kwa upande ake Qatar ilikabiliwa na tuhuma nyingi tu, lakini taifa hilo sasa liko huru kuandaa michuano hiyo.
Kwa sasa ripoti iliyotolewa na FIFA inamaliza mgogoro kuhusu ikiwa kura nyingine itapigwa kuteua waandaji wa mashindano hayo katika miaka hiyo.
FIFA imeelezea kuwa mambo sasa yako shwari kufuatia uamuzi huo.
Qatar ilituzwa kuandaa kombe la duna mwaka 2022 mnamo 2010 na kuyapiku mataifa ya Australia, Marekani,Korea Kusini na Japani.
Uamuzi ulishangaza wengi na mwishowe kupelekea madai kadhaa ya rushwa, sio tu kuhusu mchakato wa zabuni za 2022 bali pia 2018.
Urusi ilishinda zabuni ya kuandaa mashindano ya mwaka 2018 na kuishinda Uingereza ambayo ilipata kura mbili pekee.
Qatar daima imekataa madai ya kufanya kosa, lakini uchunguzi ulianzishwa ukiongozwa na mchunguzi huru wa nidhamu Michael Garcia.
Mwanasheria huyo, raia wa Amerika pia alipewa kazi ya kuchunguza michakato ya zabuni ya kombe la dunia ya 2018 na 2022.

No comments:

Post a Comment