Mmoja wa wagonjwa wanawake waliozidiwa akiwa hoi hospitalini hapo |
Ikiwa ni siku mbili baada ya kupewa huduma ya kuzuia uzazi kwa njia ya upasuaji wanawake nchini India, Daktari
anayehusishwa na tukio la vifo vya watu 13 katika kituo kilichokua
kikitoa huduma ya kuzuia uzazi kwa njia ya upasuaji jimboni Chattisgarh
nchini India,amekamatwa.
Dokta RK Gupta na msaidizi wake waliwafanyia upasuaji wananawake 83 katika kijiji cha Pendari.
Ripoti
zinasema Daktari huyo aliwafanyia upasuaji wanawake 83 kwa saa tano,
Serikali inasema Daktari mmoja anapaswa kutoa huduma ya upasuaji kwa
Watu 35 kwa siku.
Wanawake wengine wawili walipoteza maisha baada ya kufanyiwa uapsuaji huo.
Zaidi ya wanawake 90 wako hospitalini wengi wao wakiwa katika hali mbaya,baada ya upasuaji.
Maandamano
yamefanyika baada ya tukio la vifo , Serikali ya jimbo la Chhattisgarh
imetoa amri ya kufanyika kwa uchunguzi,bado haijafahamika chanzo cha
vifo hivyo.
Maafisa wa afya jimboni humo wamekana kuhusika na
tukio hilo, lakini baadhi yao wamesema walikua katika hali ya
kushinikizwa na mamlaka kufanya operesheni nyingi kwa muda mfupi.
No comments:
Post a Comment